Author Name: GlobalVoices.
(C) GlobalVoices.org
This unaltered story was originally published on GlobalVoices.org.[1]
Republishing Guidelines:
url:https://globalvoices.org/about/global-voices-attribution-policy/
--------------------



Kuokoa Maisha ya Tembo huko Laos [1]
['Mong Palatino']
Date: 2014-01-26 05:35:29+00:00

Laos hapo awali ilijulikana kama ‘ardhi ya mamilioni ya Tembo’ lakini hadi sasa idadi ya Tembo imeshapungua hadi kufikia mamia kadhaa kutokana na uwindaji haramu pamoja na biashara haramu ya pembe za ndovu. Baadhi ya tembo wanakufa kutokana na kufanyishwa kazi nyingi katika maeneo ya shughuli za ukataji na usafirishaji wa magogo.

Inakadiriwa kuwa tembo wa porini idadi yake inakadiriwa kuwa kati ya 300 hadi 600:

Wakati huohuo, kuna zaidi ya tembo 420 wanaoshikiliwa:

Inasikitisha sana kwani idadi ya Tembo wanaoshikiliwa inazidi kupungua. Kiasi cha tembo wanaoshikiliwa waliosalia Laos kinakadiriwa kuwa ni Tembo 420.Sadly captive elephant populations are in decline. Only an approximate 420 remain in Laos. Kipindi cha milenia mpya, Tembo wamekuwa wakitumika kama sehemu ya kujipatika kipato, wamiliki wa tembo hawana budi kuwatumikisha tembo wao katika siku saba za wiki ili kujikimu kimaisha. Tembo hutumiwa zaidi kwenye shughuli za usafirishaji magoo, kazi ambayo ni ngumu na hatari sana kwa tembo. Tembo wa kike huchoka sana na kushindwa kuzaa na pia huweza kupoteza maisha katika kazi za usafirishaji wa magogo.

Kwa bahati nzuri, tayari kuna ufahamu wa umuhimu wa kuwatunza Tembo katika nchi hii. Miongoni mw makundi yanayopigia chapuo harakati hizi ni Kituo cha Hifadhi ya Tembo:

Pia, kuna hospitali ya kwanza kabisa ya Tembo nchini Laos, ambapo pia, imekuwa ikitumika kama eneo la utalii la kutunza mali asili. Inatoa ushauri wa kitaalamu pamoja na namna bora ya kuishi na Tembo kwa watu wanaomiliki Tembo kwa ajili ya kujipatia kipato.

Kituo hiki pia kinatoa matunzo kwa Tembo waliojeruhiwa na kisha kuokolewa. Walishafanikiwa kumuokoa Tembo mdogo waliyempa jina la Noy. Baada ya miaka kadhaa kupita, tembo huyu atajitwalia jina jingine kupitia mchakato unaoelezewa na Afisa Mifugo afahamikaye kwa jina la Emmanuelle Chave:

Wakiwa na miaka mitatu, tembo hupata mafunzo kutoka kwa wamiliki wanaotarajia kuishi na tembo hao ya namna ya kupokea ishara mbalimbali ili kuweza kufanya kazi pamoja na binadamu.At three years old, elephants are trained by their future mahout, to respond different cues, in order to work with humans. Mzee wa kitamaduni husimamia safari hii, ambapo Tembo huacha maisha ya porini na kujiunga na maisha ya binadamu. Hadi mwisho wa mafunzo, tembo mdogo huzawadiwa miwa mitatu, ambayo juu yake kuna majina yaliyoandikwa. Jina katika mua wa kwanza atakaouchukua litakuwa lakwake.

[END]

(C) GlobalVoices
Licensed under Creative Commons Attribution 3.0 Unported (CC BY 3.0)
[1] Url: https://sw.globalvoices.org/2014/01/kuokoa-maisha-ya-tembo-huko-laos/

via Magical.Fish Gopher News Feeds:
gopher://magical.fish/1/feeds/news/globalvoices/