Author Name: GlobalVoices.
(C) GlobalVoices.org
This unaltered story was originally published on GlobalVoices.org.[1]
Republishing Guidelines:
url:https://globalvoices.org/about/global-voices-attribution-policy/
--------------------



Wanafunzi na Mwalimu Wao Watekwa Huko Kaduna Naijeria, Wakati Maharamia Wenye Silaha Wakifanya Vurugu na Mauaji · Global Voices in Swahili [1]
['Nwachukwu Egbunike']
Date: 2020-09-17 04:55:39+00:00

Maharamia wakiwa na silaha walivamia shule ya sekondari huko Kaduna, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria hapo Agosti 24 na kumuua mtu mmoja na kuwateka wanafunzi wanne na mwalimu kiliripoti chanzo cha habari za mitandaoni, SaharaReporters.

Watu hao wakiwa na silaha walifika na kushambulia kijiji cha Damba-Kasaya katika serikali ya mtaa wa Chikun, jimbo la Kaduna mnamo saa 1.45 asubuhi wakiwa kwenye pikipiki na iliripotiwa kuwa walimuua Benjamin Auta, ambaye ni mkulima, kulingana na taarifa ya gazeti la mtandaoni la Premium Times.

Watu hao wenye silaha walielekea katika shule ya sekondari ya Prince ambapo walimteka mwalim Christianah Madugu na wanafunzi wanne ambao ni Favour Danjuma, 9, Miracle Danjuma, 13, Happy Odoji, 14, na Ezra Bako, 15.

Baba yake Happy, Isiaka Odoji, aliiambia Daily Trust, gazeti la kila siku la Naijeria kwamba watekaji hao wanadai fedha kiasi cha Naira milioni 20(sawa na Dola za Marekani $53,000) ili waweze kuwaachilia huru watoto wao, lakini kamwe hawana uwezo wa kukusanya kiasi hicho.

Wanafunzi waliotekwa walikuwa wakifanya mtihani wao wa kumaliza elimu yao ya msingi. Kwa sababu ya mlipuko wa gonjwa la Korona, wanafunzi wanaomaliza shule pekee ndio waliruhusiwa kurudi shuleni.

Serikali kuu na ile ya jimbo la Kaduna zimebaki kimya kuhusu majaaliwa ya wanafunzi hao waliotekwa pamoja ma mwalimu wao.

Mtumiaji wa Twitter, Ndi Kato alisema tukio hili ni la kufadhaisha Taifa:

Today in Kaduna state, children in exit classes who were told to resume school were kidnapped by armed gunmen. One was reportedly killed. Small boy, his life cut short. The others have been taken away and we may never hear of them again.

This should devastate any nation…

— Ndi Kato (@YarKafanchan) August 24, 2020

[END]

(C) GlobalVoices
Licensed under Creative Commons Attribution 3.0 Unported (CC BY 3.0)
[1] Url: https://sw.globalvoices.org/2020/09/wanafunzi-na-mwalimu-wao-watekwa-huko-kaduna-naijeria-wakati-maharamia-wenye-silaha-wakifanya-vurugu-na-mauaji/

via Magical.Fish Gopher News Feeds:
gopher://magical.fish/1/feeds/news/globalvoices/