Author Name: GlobalVoices.
(C) GlobalVoices.org
This unaltered story was originally published on GlobalVoices.org.[1]
Republishing Guidelines:
url:
https://globalvoices.org/about/global-voices-attribution-policy/
--------------------
Mfungwa wa Zamani wa Guantanamo Ahatarisha Maisha Yake Kwa Kugoma Kula Akishinikiza Kuunganishwa na Familia Yake · Global Voices in Swahili [1]
['Fernanda Canofre']
Date: 2016-10-19 10:03:31+00:00
Jihad Diyab atahitaji magongo ya kutembelea kwa maisha yake yote yakiwa ni kitu cha kumkumbusha mateso aliyoyavumilia kwa miaka 12, miezi 8 na siku 7 kama mfungwa katika gereza la Guantanamo Bay, mahali ambapo jeshi la Marekani lilikuwa likiendesha gereza likiweka washukiwa wa makosa ya kivita kwa muda usiofahamika na bila kufunguliwa mashtaka.
Akiwa na miaka arobaini na tatu leo, Diyab amepatwa na madhara ya kudumu katika mgongo wake akiwa chini ya uangalizi wa serikali ya Marekani. Katika mahojiano yaliyafanyika mapema mwaka huu huko Uruguai, alimwambia an mwandishi wa Ki-Agentina kuwa jinamizi la Guantanamo bado linawawinda hata wafungwa waliokuwa na bahati ya kuondoka mahali hapo. Anasema kuwa “wote waliofanikiwa kutoka humo bado ni wafungwa wa Marekani kwa ndani”
Diyab ni kati ya wafungwa sita kutoka Guantanamo ( Wasyria wanne, Mpalestina mmoja na Mtunisia mmoja) ambao waliachiliwa huru na kukaribishwa nchini Uruguai hapo Disemba 2014,shukrani kwa serikali iliyofanya makubaliano kati ya Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Uruguai José “Pepe” Mujica.
Kufuatia kushindwa kwa jitihada za kuungana na familia yake, iliyokimbia kutoka Syria kwenda Uturuki, Diyab alitangaza mgomo wa kula katikati mwa mwezi Agosti. Mwezi wa tisa tarehe 15, aliliambia told shirika la habari la BBC kuwa anailaumu serikali ya Uruguai na serikali ya Marekani kwa hali aliyo nayo kwa sasa.
Mwishoni mwa Septemba, baada ya kupokea uhakika wa kuwa familia yake iko salama huko Uturuki, alianza tena kula vyakula vya majimaji .
Diyab alitengeneza vichwa vya habari mwezi Juni, alipokimbia Uruguai kupitia mpaka wa Brazili. Vyombo vya habari vya Uruguai vilimuita “muasi asiye na shukrani” kwa kuikimbia nchi iliyompokea kutoka utumwa wa Marekani. Baada ya mwezi usio na matumaini kuhusu mwenendo wake, Diyab aliibukia katika mji wa Caracas nchini Venezuela, ambapo alikamatwa na kuswekwa ndani na hatimaye kusafirishwa tena kwenda Montevideo.
Suala la kusafirishwa kwa Diyab limebaki kuwa kitendawili.Ingawa maofisa wameendelea kusema kuwa waliokuwa wafungwa wa Guantanamo ni “watu huru” ila katika uhalisia hicho kimekuwa ni kitu tofauti kabisa.
Kulingana na gazeti la Brecha,Uruguai inaonekana kukubali kuwachukua wafungwa walioachiliwa huru na kuwaweka nchini kwa miaka miwili kabla ya kutoa mguu nje ya nchi hiyo, ingawa maafisa wa serikali ya Uruguai wanakataa kuwa waliafikiana na taratibu hizo.
Mpango wowote ambao Uruguai imefanya na Washington, ukweli unabakia kuwa wafungwa walioachiliwa kutoka Guantanamo wametengenezewa kadi za uraia wa Uruguai pekee ambazo hazitafaa kusafiria katika nchi za kigeni.
Leo, mtazamo wa jamii kuhusu wafungwa wa zamani wa Guantanamo umebadilika na hata raisi wa zamani wa Uruguai aliyejadili kuhusu uhuru wa wafungwa hao kwa sasa anasema kuwa, kuwapokea hao watu ilikuwa ndio gharama nchi yake ilipaswa kulipa ili iweze kuendelea “kuuza machungwa nchini Marekani” na kuimarisha mahusiano mema.
Miezi mitano baada ya kuwasili nchini Uruguai wafungwa wanne kati ya “sita kutoka Guantanamo” walifanya maandamano mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Montevideo. Diyab hakuwepo. Wanaume hao walijikusanya mahali hapo baada ya kugundua kuwa Marekani imekataa kuwapa msaada wa fedha.
Wakiandika katika blogu,wanaume hao wanasema kuwa wametelekezwa katika nchi ya kigeni bila ajira, bila familia zao au uelewa wa lugha ya asili ya mahali hapo. Kwa hili, na kwa miaka 13 waliyotumikia wakiwa wamefungwa bila mashtaka, wanastahili msaada kutoka kwa serikali inayowajibika, waliyasema hayo hapo April:
They [the U.S.] Wanatakiwa watupe namna ya kuishi kama binadamu wengine. Hawawezi kurusha makosa kwa watu wengine, wangetusaidia nyumba na misaada ya kifedha. Hatuombi yasiyowezekana kutoka kwao, walitufunga kwa miaka 13 hivyo wangepaswa kutusaidia kwa miaka kadhaa ijayo. Tunafikiri kuwa hiki ni kitu kidogo tu wanachoweza kufanya au tunachowaomba.
[END]
(C) GlobalVoices
Licensed under Creative Commons Attribution 3.0 Unported (CC BY 3.0)
[1] Url:
https://sw.globalvoices.org/2016/10/mfungwa-wa-zamani-wa-guantanamo-ahatarisha-maisha-yake-kwa-kugoma-kula-akishinikiza-kuunganishwa-na-familia-yake/
via Magical.Fish Gopher News Feeds:
gopher://magical.fish/1/feeds/news/globalvoices/